Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbeto ajigamba hakuna chama cha kuzuia Ushindi wa CCM 2025

  • 28
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi kimesema bado hakijatokea chama cha Siasa makini chenye uwezo na sera za kuzuia ushidi wa CCM katika chaguzi Kuu zote za Tanzania na Zanzibar Oktoba Mwaka huu.

CCM pia kimeahidi kushinda chaguzi kuu zote Zanzibar na Tanzania kutokana na ubora wa Sera zake, mikakati yake , Ognaizesheni ya chama ,Ilani yake mpya na maandalizi ya nyenzo za kampeni.

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar ,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo,Khamis Mbeto Khamis, alipohojiwa na Waandishi wa habari baada ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Samia Suluhu kuweka Jiwe la Msingi la Makao Makuu ya CCM jijinj hapa .

Mbeto alisema Ushindi wa CCM utatokana na Utekelezaji wa Sera zake kupitia ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 na kuzinduliwa kwa ilani mpya ya Mwaka 2025 -2030.

Alisema kazi kubwa ya kukamilkisha Miradi ya Maendeleo iliofanywa na Marais , Dk Samia na Dk Hussein Ali Mwinyi, zimefanyika kwa Viwango vya Juu na kuleta ufanisi wa aina yake.

“Mtaji mkubwa wa ushindi wa CCM,kwanza hutokana na idadi ya Wanachama wake Milioni 13 nchi nzima. Utekelezaji wa Sera zake na kukamilika miradi ya kimkakati ambayo ni tiketi ya ushindi kwa CCM ” Alisema Mbeto.

Katibu huyo Mwenezi wa Kamati Maalum NEC Zanzibar , alisema Rais Dk Samia , ameliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa ya Kiuchumi na Maendeleo yanayoonekana , ikiwemo kuacha alama ya kihistoria kujenga Jengo la Makao Makuu ya CCM.

Aidha ,alisema chini ya Uongozi wa CCM na Serikali zake, Tanzania imeendelea kujijenga katika Siasa za Kimataifa kupitia diplomasia yake ya Uchumi na kuendeleza Ushirikiano wa Kimataifa .

“Maendeleo yanaonekana katika kila kona ya Tanzania na Zanzibar hajawahi kutokea. Kazi ya kutumikia wanachi imefanyika kwa viwango na utekelezaji wa Miradi ya kisekta na Maendeleo kwa Miji na vijijini vyote “Alieleza.

Pia alisema chini ya Uongozi wa Marais hao, Tanzania na Zanzibar zimeendelea kuaminiwa na Taasisi mbalimbali za Fedha Duniani, huku ikipatiwa mikopo iliosaidia kusukuma mbele maendeleo nchini .

“Kutokana na usimamizi makini wa Sera za chama na Ilani Serikali zetu zimetimiza wajibu wake kwa kipindi cha Mwaka 2020 -2025. Mkutano Mkuu wa CCM hapa Dodoma utazindua ilani mpya ya Mwaka 2025-2030 .Ni ilani ya maendekeo makubwa yajayo “Alisisitiza katibu Mwenezi huyo.

“CCM hakitashindwa Uchaguzi na Vyama visivyo na malengo ya sera wala Ilani za Uchaguzi .Kazi ya kujenga chama cha siasa kinachobeba matumaini ya Wananchi ni kazi inayohitaji uthubutu, akili na maarifa “Alisema Mbeto.



Prev Post Waziri Mkuu Majaliwa Akutana Na Waziri Mkuu Wa Japan
Next Post Bodi ya Ligi Yathibitisha Dabi ya Kariakoo Kuchezwa Juni 15, 2025 – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook