

Kada maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob almaarufu Boni Yai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya chama hicho, amesema mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Freeman Mbowe hahusiki kwa namna yoyote na wanaojitoa kwenye chama hicho.

Boni Yai ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mei 18, 2025.
Hata hivyo ameeleza kuwa baadhi ya mambo yanayoendelea juu ya kukipinga chama hicho na misimamo yake pamoja na uongozi hayana baraka za Mbowe.
Kuithibitisha hilo Boniface ameeleza kuwa yeye binafsi Mbowe alimuarifu kuwa amezungumza na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika na mazungumzo yao ilikuwa juu ya kama Mbowe anabariki mienendo ya baadhi ya watu wanaopinga msimamo wa chama.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!