Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Askofu Novatus Rugambwa Kuagwa Dar, Kuzikwa Bukoba

  • 1
Scroll Down To Discover

Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imetangaza ratiba ya kuaga na mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa aliyefariki dunia Septemba 16, 2025 huko Roma, Italia.

TEC imesema Askofu Rugambwa, aliyewahi kuwa Balozi na Baba Mtakatifu huko New Zealand, atakumbukwa kwa utumishi wake wa muda mrefu kwa Kanisa Katoliki na Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Clement Kihiyo, misa ya kumuaga itafanyika Jumamosi, Septemba 27, 2025 saa 3:00 asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam. Misa ya mazishi itafanyika Jumatatu, Septemba 29, 2025 saa 3:30 asubuhi katika Kanisa Kuu Jimboni Bukoba.

TEC imewaomba waamini wote waendelee kumuombea Askofu Mkuu Rugambwa na familia yake.

“Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie. Apumzike kwa Amani, Amina,”



Prev Post Binti wa Rais Paul Biya Aomba Umma Wasimpigie Kura Baba Yake
Next Post Mwenyekiti wa NEC Jaji Mwambegele Akagua Maandalizi ya Uchaguzi Mbeya
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook