Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KOCHA YANGA AMTAJA ALIYEIOKOA SIMBA NA KIPIGO CHA AIBU JUZI….

  • 9
Scroll Down To Discover

KIWANGO bora alichoonyesha kipa wa Simba, Moussa Camara ‘Spiderman’ katika pambano la Dabi ya Kariakoo, kimemshtua kocha Mfaransa anayeinoa Yanga na kusema kama sio umahiri wa kipa huyo raia wa Guinea, huenda mambo yangekuwaharibikia Wanamsimbazi.

Katika pambabo hilo la Ngao ya Jamii lililochezwa Jumanne ya wiki hii, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, huku Camara akiokoa michomo kadhaa ya wazi ya Yanga na kumfanya kocha Romain Folz, ashindwe kujizuia na kumwagia sifa kipa huyo wa timu pinzani mara baada ya mechi.

Folz, raia wa Ufaransa aliyeiongoza Yanga kwa mara ya kwanza katika mechi za mashindano na ya kwanza dhidi ya Simba na kuibuka na ushindi huo, alionekana akimfuata Camara mara baada ya mchezo huo na Mwanaspoti lilimtafuta kipa hiyo aliyefichua alichozungumza.

Camara alisema kocha huyo aliyechukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyeondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akiipa timu hiyo mataji matatu, Kombe la Muungano, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, alimpongeza kwa umahiri akisema kama sio yeye SDimba ingepigwa nyingi.

“Kocha wa Yanga alifurahishwa na kiwango changu, jinsi ambavyo nimepangua mashambulizi ya viungo na washambuliaji wa timu hiyo na aliniambia hata baada ya kunifuata mara mechi ilipomalizika,” alisema Camara na kuongeza;

“Kweli haukuwa mchezo mwepesi kabisa, hilo lazima ni liweke wazi unajua unapokutana na Yanga ni timu kubwa, hivyo licha ya kuruhusu bao moja lakini nimefurahi kocha wao ameona ubora wangu. Ila niseme wazi pongezi zile za kocha zinaenda kwa kikosi kizima, kwani naona tuna timu bora iliyopunguza makosa mengi tofauti na wakati uliopita, kwangu naona tunazidi kuwa bora na yajayo yanafurahisha.”

BAADA YA DABI

Camara alisema mara baada ya mechi hiyo akili yake sasa imehamia katika michuano ya kimataifa ambapo kesho watakuwa ugenini kuvaana na Gaborone United ya Botswana.

“Kwa sasa tunaziangalia mechi za kimataifa zilizopo mbele yetu kama unavyojua Simba sio timu yenye malengo madogo. Msimu huu hatutaki kuishia njiani malengo yetu ni kufika fainali za Ligi ya Mabingwa kabisa, maana msimu uliopita tulifika ya Shirikisho,” alisema Camara aliyemaliza kinara wa clean sheet (19) katika Ligi Kuu na namba mbili wa michuano ya CAF kwa msimu uliopita.

“Naamini hilo tutalifanikisha na kwenye ligi pia huu msimu hatutamuachia Kombe yoyote, hayo ni malengo ya timu na yangu, hivyo wapinzani wa jipange,” aliongeza Camara.

The post KOCHA YANGA AMTAJA ALIYEIOKOA SIMBA NA KIPIGO CHA AIBU JUZI…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KWA HALI HII…YANGA WANAKAZI YA KUFANYA ANGOLA LEO…WAKIKAA VIBAYA TU CHALII….
Next Post Jiko Linalotumia Mfumo wa Nishati Safi Lazinduliwa Sekondari Yusuf Makamba
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook