Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mawakili wa Serikali Watakiwa Kuzingatia Sheria za Hifadhi ya Jamii

  • 3
Scroll Down To Discover

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari afungua mafunzo ya hifadhi ya jamii kwa Mawakili wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari afungua mafunzo ya hifadhi ya jamii kwa Mawakili wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amewataka Mawakili wa Serikali kuyatumia mafunzo yanayotolewa kuhusu Hifadhi ya Jamii, katika kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni za Hifadhi ya Jamii zinalinda na kusimamia haki na maslahi ya Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Johari alitoa wito kwa Mawakili wa Serikali wanaoshiriki mafunzo hayo kuwa na ari  na kuhakikisha kuwa maarifa watakayoyapata wanayaweka katika Vitendo na kuhakikisha kuwa PSSSF inaendeshwa kwa ufanisi na kwa mujibu wa Sheria na Kanuni.

“ Wajibu wetu ni  kuhakikisha kuwa PSSSF inaendeshwa kwa ufanisi na kwa mujibu wa sheria na kanuni, na hivyo kulinda haki za wanachama wake.” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Uongozi kwa kuandaa na kufadhili mafunzo hayo kwa Mawakili wa Serikali kwakuwa yatawasaidia  kupata uelewa wa kitaalamu na kisheria ili kuongeza weledi katika sheria, usimamizi na uendeshaji wa shughuli za Hifadhi ya Jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa PSSSF Vupe Ligate amesema kuwa wanaendesha mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Hifadhi ya Jamii ambayo yatawarahisishia utendaji kazi wao wakati wakitoa ushauri wa Kisheria  kuhusiana na Hifadhi ya Jamii.



Prev Post DC Nyamagana: Serikali Inatambua Kazi Nzuri ya OSHA Nchini
Next Post NBC Yazindua Msimu wa nne wa Kampeni ya NBC Shambani Kwa Wakulima wa Korosho Mtwara
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook