
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na mikutano yake ya kampeni katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Dkt. Samia alizungumza na wananchi wa Makunduchi, Zanzibar, mnamo tarehe 17 Septemba 2025, akisisitiza dhamira ya CCM kuendeleza maendeleo ya wananchi na kulinda mshikamano wa kitaifa.
Ziara hii ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!