

Dar es Salaam imekumbwa na simanzi kubwa kufuatia ajali mbaya iliyopoteza maisha ya Baba wa familia, Francis Elineema Kaggi, watoto wake watatu – Joshua Francis Kaggi, Janemary Francis Kaggi na Maria Francis Kaggi – pamoja na ndugu yao Elineema Hamisi Kaggi. Ajali hiyo imemuacha mke wa marehemu, Sophia Kaggi, akiwa hai lakini akishuhudia familia yake ikipoteza maisha mbele ya macho yake.
Shuhuda wa tukio hilo amefunguka kupitia Global TV, akisimulia namna ajali hiyo ilivyotokea. Kwa mujibu wake, gari walilokuwa wakisafiria familia ya Kaggi lilipoteza mwelekeo ghafla baada ya kurejea kutoka Tanga, walipokuwa wamehudhuria msiba wa mama wa shemeji yao. Shuhuda huyo alieleza kuwa sekunde chache baada ya kelele za breki, gari lilipinduka na kugonga kwa nguvu, jambo lililosababisha vifo vya papo hapo vya baadhi ya abiria waliokuwemo ndani.
Mwili wa marehemu Francis Kaggi na watoto wake uliagwa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, ambapo mamia ya waombolezaji walijitokeza kushuhudia na kutoa heshima za mwisho. Wengi waliomboleza familia hiyo wakieleza kuwa walikuwa mfano wa mshikamano na upendo wa kifamilia.
Ajali hii imetikisa sio tu ndugu na jamaa wa familia ya Kaggi, bali pia jamii nzima, ikibaki kama kumbukumbu ya majonzi kwa waliowahi kuwatambua.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!