Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mmoja Auawa Kwa Kisu Kisa Simba, Yanga

  • 3
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limethibitisha mauaji yaliyotokea Septemba 16, 2025 saa 12:50 jioni Kitongoji cha Ululu, Idiwili – Mbozi.

Evaristo Zabroni Mwambogolo (28) alichomwa kisu kifuani na Exavery Jamsoni Mwaweza baada ya mabishano ya mpira wa miguu kati ya mashabiki wa Simba na Yanga. Marehemu alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Zahanati ya Lyula. Mtuhumiwa ametoroka na msako mkali unaendelea.

Aidha, Septemba 15, 2025 saa 03:00 asubuhi, barabara ya Tunduma–Sumbawanga (eneo la Nyerere), gari Canter T.525 ACB liligonga bajaji MC 308 EXE na kusababisha vifo vya watu watatu akiwemo Silas Malongo (23) na majeruhi wawili. Dereva wa Canter alikimbia na msako unaendelea.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kudumisha amani na kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.



Prev Post Makunduchi Wamkaribisha Dk. Samia Kwa Kishindo
Next Post Ajali Iliyochukua Maisha ya Baba na Watoto: Shuhuda Aeleza Dakika za Mwisho
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook