
15 Septemba 2025 – Xiaomi, moja ya kampuni vinara wa ubunifu wa kiteknolojia duniani, imeingia rasmi katika soko la Tanzania kwa kuzindua simu yake mpya ya kisasa, Redmi 15C. Hatua hii ni ishara ya mchango wa Tanzania katika kuwa kitovu cha matumizi ya kidijitali katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Tanzania: Soko Linalokua kwa Kasi, Ujio wa Xiaomi unaonesha imani ya chapa hiyo katika ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini Tanzania. Ikiwa na idadi kubwa ya vijana na ongezeko la matumizi ya intaneti ya simu, Tanzania ni fursa ya kipekee kwa ubunifu na maendeleo.
Uzinduzi wa Redmi 15C ni kielelezo cha dhamira ya Xiaomi kuhakikisha teknolojia ya kisasa inapatikana kwa vijana na sekta ya biashara nchini.
Bw. Eric William Mkomonye, Meneja Masoko wa Xiaomi Tanzania, alisema:
“Tanzania ni moja ya masoko yenye hamasa kubwa Afrika Mashariki, yenye idadi kubwa ya vijana wanaoongoza mabadiliko ya kiteknolojia. Kupitia Redmi 15C, tunawaletea kifaa kinachochanganya urahisi, uimara na ubunifu kwa bei inayoendana na mazingira ya soko. Aidha, tunatoa dhamana ya miezi 24 + 1 kwa kila kifaa, ikiwa ni ya kwanza
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!