
Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Mzee Yusuf Makamba amewaomba wananchi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mhandisi Ramadhani Singano na madiwani wote wa chama hicho.
Makamba amesema hayo leo Septemba 15, 2025 kwa njia ya simu kwenye mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika Lushoto eneo la Soni.
Mzee makamba amesema anaimani na wagombea wote wa CCM na alipenda kuhudhuria mkutano huo ila tatizo ni changamoto ya afya yake.
Dk Nchimbi alimpigia simu Mzee Makamba akiwa jukwaani ndipo alipozungumza na kuwaombea kura wagombe wote huku akiwaomba wananchi wa mkoa wa Tanga wasimuangushe katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!