Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wafanyabiashara 186 Wahitimu Mpango wa Maendeleo ya Usambazaji Bidhaa

  • 3
Scroll Down To Discover

Mhe. Dkt. Blandina Kilama, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa mahafali ya Supplier Development Programme (SDP) yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam.

Wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs) wa Kitanzania wamehitimu kwenye Mpango wa Maendeleo ya Usambazaji bidhaa kwa kujengewa ujuzi na mitandao ya kushindana katika minyororo ya usambazaji ya kampuni, serikali na masoko ya kikanda chini ya AfCFTA.

Ushirikiano na GAIN umeleta mkondo maalum unaojikita katika kusambaza lishe, kwa kusaidia biashara za chakula na kilimo ambazo si tu zinakua kibiashara bali pia kuboresha upatikanaji wa chakula bora na nafuu nchini Tanzania.

Serikali, sekta binafsi na washirika wa maendeleo wameungana katika Mkutano wa Kwanza wa Biashara wa Stanbic kujadili mchango wa maudhui ya ndani katika kufanikisha Dira ya 2050, kwa kulinganisha maendeleo ya biashara na malengo ya kitaifa na kimataifa.

Dar es Salaam, Tanzania – Ijumaa, 12 Septemba 2025: Wafanyabiashara ndogo na za kati (SMEs) 186 wa Kitanzania wamehitimu mafunzo yao kwenye Mpango wa Maendeleo ya Wasambazaji (SDP) wakati wa Mkutano wa kwanza wa Biashara wa Stanbic uliofanyika jijini Dar es Salaam, tukio ambalo viongozi wamelipongeza kama hatua muhimu kwa ujasiriamali, lishe na ukuaji jumuishi.

Tukio hilo, lililofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, liliunganisha sherehe ya mahafali na mjadala wa ngazi ya juu kuhusu jinsi maudhui ya ndani yanavyoweza kuendesha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania. Maafisa wa serikali, viongozi wa sekta binafsi, washirika wa maendeleo na wajasiriamali walihudhuria sherehe hiyo, ambayo waandaaji walisema itakuwa jukwaa la kila mwaka la maendeleo na ubunifu wa biashara.

Darasa la wahitimu wa 2025 lilihusisha wafanyabiashara 186 kutoka makundi manne, zikiwemo biashara zilizoshiriki katika mkondo maalum wa lishe kwa kushirikiana na Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN). Hii inaleta jumla ya wahitimu kufikia 300 tangu kuanzishwa kwa programu mwaka 2022.

SDP inawawezesha SMEs kwa stadi za vitendo katika usimamizi wa kifedha, uongozi, kufuata taratibu za minyororo ya usambazaji, uhusiano wa masoko na ubunifu.

Washiriki sasa wako tayari zaidi kushindania mikataba na makampuni makubwa, taasisi za serikali na

masoko ya kikanda chini ya Mkataba wa Biashara Huru wa Bara la Afrika (AfCFTA).

“Mpango huu unafunga pengo kati ya matarajio na fursa,” alisema Kai Mollel, Mkuu wa Stanbic Biashara Incubator, anayesimamia mpango huo. “Unawasaidia wajasiriamali kuhamia kutoka kwenye uendeshaji usio rasmi hadi kuwa biashara zilizo tayari kupokea uwekezaji na kushiriki katika minyororo mikubwa ya usambazaji.”

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Blandina Kilama, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango alisifu mchango wa programu hii kwa mustakabali wa uchumi wa Tanzania. “SMEs ndizo uti wa mgongo wa uchumi wetu. Barani Afrika zinatoka zaidi ya asilimia 70 ya ajira na kuchangia hadi asilimia 40 ya Pato la Taifa (GDP),” alisema.

“Kwa kuimarisha SMEs, tunaimarisha Tanzania yenyewe. Kinachonifurahisha zaidi ni kwamba baadhi ya wahitimu hawa hawajengi biashara pekee bali pia wanatatua changamoto za lishe na usalama wa

chakula.”

Mkutano huo uliambatana na maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya Stanbic nchini Tanzania. Afisa Mkuu wa Fedha na Thamani, Derick Lugemala alisema mkakati wa benkihiyo unaenda zaidi ya fedha na unalenga kujenga biashara zinazoshindana.

“Kwa miongo mitatu, tumekuwa zaidi ya benki; tumekuwa mshirika katika safari ya ukuaji wa Tanzania,” alisema. “Kupitia Biashara Incubator, tunajenga mtiririko wa SMEs zilizo tayari kupanuka,

kupata mikataba na kusambaza kikanda.

Kwa ushirikiano na GAIN, tunaonyesha kuwa ukuaji wa biashara na athari chanya kwa jamii vinaweza kwenda sambamba.”

Aliongeza kuwa mkondo wa lishe unahusiana moja kwa moja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, hususan Kutokomeza Njaa, Afya Njema na Usawa wa Kijinsia.

Mpango wa Maendeleo ya Wasambazaji ni zaidi ya mahafali; ni kuhusu kujenga mustakabali bora kwa Watanzania. Kwa kuwapa biashara ndogo zana za kukua, unasaidia kuunda ajira kwa familia, kuimarisha minyororo ya usambazaji wa ndani inayosogeza bidhaa na kuwapa wajasiriamali ujasiri wa kushindana nje ya mipaka yetu.

Kupitia mkondo wa lishe, biashara hizi pia zinasaidia watu wengi zaidi kupata chakula bora kwa bei nafuu.

Hii inaonyesha kuwa kukuza biashara pia kunaweza kumaanisha kukuza jamii imara – mtazamo

unaoipeleka Tanzania karibu na malengo yake ya muda mrefu chini ya Dira ya 2050.

Ushirikiano na GAIN umejikita katika biashara za kilimo na mifumo ya chakula, ukiwa na lengo la kufanya chakula chenye lishe kipatikane zaidi. “Biashara zinazojali lishe ndizo msingi wa kuunda jamii zenye afya njema,” alisema Dkt. Winfrida Mayila, Mkuu wa Programu, GAIN Tanzania.

“Kwa kusaidia SMEs katika sekta hii kukua, tunachangia maendeleo ya kiuchumi pamoja na kuboresha afya ya Watanzania.”

Miongoni mwa mambo muhimu katika Mkutano huo ilikuwa mjadala wa paneli wenye mada: “Maudhui ya Ndani kama Kichocheo cha Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi – Kuelekeza Biashara za Kitanzania Zinazoshindana kuelekea Dira ya 2025.”

Wajumbe wa paneli, wakiwemo maafisa waandamizi wa serikali na wajasiriamali, walijadili jinsi

wasambazaji wa ndani wanaweza kuchukua nafasi kubwa zaidi katika maendeleo ya taifa kwa kutimiza viwango vya ununuzi, kuleta ubunifu na kushindana kikanda.

Waandaaji walisema kuwa Mkutano wa Biashara utakuwa tukio la kila mwaka la kuonyesha ujasiriamali, kuhamasisha mjadala wa sera na kusherehekea ubunifu wa biashara.

Kwa wajasiriamali waliokuwa wakihitimu, sherehe hiyo haikuwa mwisho bali mwanzo. Kama mshiriki mmoja alivyosema: “Mpango huu umetupa ujasiri wa kushindana.

Sasa ni juu yetu kutumia tulichojifunza na kujenga biashara zinazounda ajira, kukuza kipato na kuifanya Tanzania ijivunie.”



Prev Post Mahakama Kuu Yaikataa Mapingamizi ya Lissu Katika Kesi ya Uhaini
Next Post Serikali Yawataka Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuhakikisha Miradi Wanayosimamia Inakidhi Viwango
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook