Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Pingamizi la Mwanasheria Mkuu Lamng’oa Mpina Uchaguzi wa Urais 2025

  • 2
Scroll Down To Discover

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuondoa jina la Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, katika orodha ya wagombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam Septemba 15, 2025 na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, hatua hiyo imechukuliwa baada ya INEC kukubali pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Saidi Johari, dhidi ya uteuzi wa Mpina.

Tume katika kikao chake kilichofanyika tarehe 15 Septemba, 2025 imefanya uamuzi wa mapingamizi hayo manne (04) yaliyowasilishwa mbele yake, ambapo mapingamizi matatu (03) yamekataliwa na moja limekubaliwa”, ameeleza Kailima.

Mapingamizi yaliyokataliwa ni la Almas Hassan Kisabya (mgombea Urais wa NRA) dhidi ya Luhaga Mpina (ACT Wazalendo), na la Kunje Ngombale Mwiru (mgombea wa AAFP) dhidi ya Mpina na pingamizi la Mpina dhidi ya uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan (CCM).

INEC imeeleza kuwa kwa uamuzi huo, jina la Mpina limeondolewa rasmi kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, huku wagombea wengine waliowasilisha majina yao wakibaki kuendelea na mchakato.

Tume imesisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 na Kanuni ya 22 ya Kanuni za Uchaguzi wa mwaka 2025.



Prev Post Burkina Faso Yapunguza Sikukuu za Umma Kuokoa Bilioni 17
Next Post Jeshi la Polisi Lamuita Polepole Kutoa Ushahidi wa Tuhuma
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook