Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Burkina Faso Yapunguza Sikukuu za Umma Kuokoa Bilioni 17

  • 9
Scroll Down To Discover

Waziri wa Utumishi wa Umma, Mathias Traore

OUAGADOUGOU – Serikali ya Burkina Faso imewasilisha muswada wa kupunguza idadi ya sikukuu za kitaifa kutoka 15 hadi 11, hatua inayolenga kuokoa takribani faranga za CFA bilioni 17 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Waziri wa Utumishi wa Umma, Mathias Traore, kila siku ya mapumziko yenye malipo hugharimu Serikali takribani faranga bilioni 4 za CFA, hali inayochangia upotevu wa zaidi ya bilioni 67 CFA kwa mwaka 2025 (sawa na zaidi ya Euro milioni 100).

Sikukuu zitakazopunguzwa ni pamoja na kumbukumbu ya uasi wa Januari 3, kutangazwa kwa uhuru Agosti 5, Siku ya Wafiadini Oktoba 31, tarehe ya kupinduliwa kwa Blaise Compaoré, na Jumatatu ya Pasaka. Tatu kati ya siku hizo zimeainishwa kama za ukumbusho wa kihistoria.

Serikali inasema hatua hiyo inalenga kupunguza mzigo wa kifedha kwenye bajeti na kuongeza ufanisi wa kiuchumi.

KATIBU TAWALA AKOSHWA na SHARIFA ALIYEANZISHA VIKOBA MIAKA 10 ILIYOPITA – AFUNGUKA…



Prev Post Waziri Mkuu Awataka Wana-Lindi Kumchagua Dkt. Samia Oktoba 29
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook