Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Trump Ataka NATO Kusitisha Ununuzi wa Mafuta ya Urusi

  • 2
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameongeza shinikizo kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Kijeshi ya NATO kwa kuwataka kusitisha mara moja ununuzi wa mafuta na gesi kutoka Urusi, pamoja na kuweka ushuru mkubwa kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China.

Kwa mujibu wa Trump, hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa kuimaliza haraka vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, ambayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa na kuyumbisha uchumi wa dunia.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika Ikulu ya White House leo Jumamosi, Trump alieleza kuwa Marekani iko tayari kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya Moscow, lakini akasisitiza kwamba ufanisi wa hatua hizo utategemea mshikamano wa pamoja wa wanachama wote wa NATO.

“Iwapo mataifa ya NATO yatashirikiana nasi kwa dhati, tunaweza kuiwekea Urusi vikwazo vizito vitakavyosababisha shinikizo kubwa la kiuchumi na kisiasa. Hii itaisukuma Urusi kukubali masharti ya amani na kuacha uvamizi wake dhidi ya Ukraine,” alisema Trump.

Aidha, Trump alibainisha kuwa hatua ya kuwekea ushuru mkubwa bidhaa kutoka China inalenga kuipunguza nguvu Beijing, ambayo inashutumiwa kwa kuunga mkono Urusi kwa njia zisizo za moja kwa moja kupitia biashara na ushirikiano wa kiuchumi. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kudhoofisha nafasi ya China kutapunguza uwezo wake wa kuisaidia Urusi, hali ambayo anaamini inaweza kuharakisha kumalizika kwa vita hiyo.

Hata hivyo, Trump alitoa onyo kali akisema kuwa iwapo nchi za NATO hazitaungana na Marekani katika utekelezaji wa hatua hizo, jitihada zote zitakuwa bure na kuishia kupoteza muda na rasilimali. “Tunapigania si tu usalama wa Ukraine, bali pia uthabiti wa dunia nzima. Kila siku vita inapodumu, maisha mengi yanapotea, na gharama kwa walipa kodi zinazidi kupanda. Ni lazima tuonyeshe mshikamano na kuchukua hatua za pamoja sasa,” alisisitiza.

STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL

”NAPENDA UIGIZAJI WA ELIUD – MBONA HUJANIALIKA DADA’AKO KWENYE HARUSI” – MATUMAINI WA KIWEWE…



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 14, 2025
Next Post Dkt. Mwinyi Azindua Kampeni za CCM Zanzibar kwa Kishindo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook