Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Nepal: Vifo vya Maandamano Vyafikia 51, Jaji Mkuu wa Zamani Aongoza Serikali ya Mpito

  • 5
Scroll Down To Discover


Polisi Nepal imesema idadi ya vifo imeongezeka kutokana na maandamano ya wiki hii huku Rais wa nchi hiyo na mkuu wa majeshi wakitarajiwa kufanya mkutano muhimu hii leo.

Msemaji wa polisi nchini Nepal, Binod Ghimire amesema kuwa idadi ya vifo kutokana na maandamano yaliyofanyika wiki hii nchini humo imefikia watu 51. Watu hao wakiwemo waandamanaji 21, wafungwa tisa, maafisa watatu wa polisi na raia wengine 18 walifariki kutokana na maandamano hayo kupinga ufisadi.

Inaarifiwa pia kuwa karibu wafungwa 12,500 walitoroka gerezani hadi sasa bado wanasakwa. Hizo zilikuwa ghasia mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa huko Nepal tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukomeshwa kwa utawala wa kifalme mnamo mwaka 2008.

Rais wa Nepal Ramchandra Paudel na mkuu wa majeshi Jenerali Ashok Raj Sigdel walitarajiwa kutafanya mkutano muhimu jana Ijumaa ambao uliwashirikisha wadau mbalimbali ili kumteua kiongozi wa mpito atakayekubaliwa na pande zote kwa ajili ya kuziba ombwe la utawala baada ya maandamano makubwa yaliyoiangusha serikali na kuliacha bunge likiwaka moto.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na mwandamanaji Kamal Giri, leo Jaji mkuu wa zamani ndiye ametangazwa kuwa kiongozi wa mpito. “Ili kutafuta suluhisho kutokana na hali ya sasa, mkuu wa majeshi na rais wameafiki kumteua jaji mkuu wa zamani Sushila Karki kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito, na hili ni jambo la kupongezwa sana.”

Sushila Karki ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza wa Nepal kuteuliwa katika nafasi hiyo mwaka 2016 atasaidiwa na mwanaharakati mkuu wa kundi la vijana wanaofahamika zaidi kama “Gen Z” ambao ndio walikuwa mstari wa mbele kwenye maandamano hayo.

Wakati baadhi ya vijana wakishinikiza pia kuvunjwa kwa Bunge, Rais Paudel ametoa taarifa kwa umma hapo jana jioni akisema kuwa “suluhisho la tatizo hilo linashughulikiwa haraka iwezekanavyo.” Jeshi limeendelea kushika doria katika mitaa yenye utulivu ya mji mkuu Kathmandu kwa siku ya tatu mfululizo.

Taifa la Nepal lenye watu milioni 30 lilitumbukia katika machafuko makubwa wiki hii baada ya vikosi vya usalama kujaribu kusambaratisha mikusanyiko ya vijana waliokuwa wakiandamana kupinga ufisadi na kufungwa kwa mitandao ya kijamii.

Maandamano hayo yalipelekea Waziri Mkuu Khadga Prasad Oli kujiuzulu na kukimbia.

STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL



Prev Post Mpina Arejesha Fomu za Urais ACT-Wazalendo Baada ya Uamuzi wa Mahakama
Next Post Bosi Wangu Alitaka Kuniangamiza Kwenye Kazi, Lakini Hatua Niliyopiga Ilimfanya Aniombe Msamaha
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook