Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

‎Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania Aweka Jiwe La Msingi Shule Ya Polisi Jeshi Mafinga

  • 13
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 12  Septemba 2025  ameweka  jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Polisi Jeshi katika kijiji cha Mkanzaule Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa.
‎Akizungumza wakati wa sherehe hizo,  Jenerali Mkunda alisema kuwa kwa upande wa Jeshi ni historia na ni mara ya kwanza kwa Polisi Jeshi kuwa na shule yao ya kujitegemea huku akimshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono uboreshaji wa miundo mbinu ya mafunzo jeshini.
Pia alisema uamuzi wa kujenga shule hiyo ni jawabu mojawapo la kuhakikisha Polisi Jeshi wanapata mafunzo yenye utaalamu wa kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya kipolisi kwa weledi mkubwa na ufanisi mkubwa.
‎Aidha, akizungumza mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi, Jenerali Mkunda amewaasa Maafisa na Askari kuviishi viapo vyao wakati wote wanapotekeleza majukumu ya kijeshi.



Prev Post Majaliwa Azindua  Kampeni Za Ubunge Jimbo  La  Nachingwea
Next Post Tanesco Yapiga Marufuku Wizi na Uharibifu wa Miundombinu ya Umeme
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook