
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, pamoja na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo hilo, Paul Ruzoka, katika Ikulu Ndogo ya Tabora tarehe 12 Septemba, 2025.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wa Kanisa Katoliki walipata nafasi ya kubadilishana mawazo na Rais Samia kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kijamii. Aidha, maaskofu hao walimwombea dua na baraka Rais Samia ambaye ni mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!