
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumza na maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, akieleza mipango mikubwa ya maendeleo endapo CCM itaendelea kushika dola katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika mkutano huo uliofanyika Septemba 11, 2025, Dkt. Samia aliahidi miradi kadhaa ikiwemo:
-
Ujenzi na uendelezaji wa vituo vya afya.
-
Kuendeleza barabara kwa kiwango cha lami na changarawe ili kurahisisha mawasiliano.
-
Ujenzi wa mabwawa na maboresho ya miundombinu ya umwagiliaji.
-
Kuimarisha mradi wa “Build a Better Tomorrow – BBT” kwa mashamba ya kilimo na ufugaji kwa vijana.
-
Ujenzi wa chujio la maji bwawa la Ichemba na kufikisha maji safi katika vijiji 17.
-
Uchimbaji wa visima vipya vya maji katika maeneo ya Kaliua.
-
Kuanzisha shamba la malisho pamoja na kujenga mnada na machinjio ya kisasa.
Kuhusu sekta ya afya, Dkt. Samia alisema serikali yake itahakikisha hospitali ya wilaya ya Kaliua inakamilika, ikiwemo majengo ya huduma kwa mama na mtoto ambayo hayajakamilika.
Rais Samia alihitimisha mikutano yake ya kampeni kwa siku ya Septemba 11 mkoani Tabora, na anatarajiwa kuendelea na ratiba yake kesho.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!