
Mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kuwa endapo Watanzania watampa ridhaa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano, serikali yake imedhamiria kuboresha elimu kwa kujenga sekondari mpya 11 pamoja na madarasa mapya 98 katika Halmashauri ya Mlele, mkoani Katavi.
Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo leo, Septemba 10, 2025, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Halmashauri ya Mlele, Dkt. Nchimbi akiendelea kunadi sera za CCM, amesema chama hicho pia kimedhamiria kutekeleza miradi 16 ya maji safi na salama katika eneo hilo.
“Sambamba na hayo, kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025–2030, tutaendelea kuboresha hali ya barabara pamoja na miundombinu mbalimbali kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya wananchi,” amesema Dkt. Nchimbi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!