

Chama cha CHAUMMA katika Jimbo la Segerea, kumezidi kuwaka. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia makundi ya wanachama kuzidi kukihama chama hicho kwa madai ya kutoridhishwa na mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Agnesta Kaiz.
Baadhi ya waliokuwa viongozi wa CHAUMMA ngazi ya mabaraza katika kata za Vingunguti, Minazi Mirefu, Kipawa na Kimanga, katika jimbo hilo jana wametangaza kujiunga na CHADEMA wakidai chanzo ni kutoridhishwa na mgombea huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapokea wanachama hao aliyekuwa Mwenyekiti wa CHAUMMA Kata ya Kinyerezi, Mlewa Juma Mlewa ‘Dk.Timo’ alisema kuna idadi kubwa ya wanachama chama hicho watajiunga na vyama vingine kutokana na kutomkubali mgombea huyo wa CHAUMMA.
“Ninawaambia ukweli Segerea,mgombea huyu wa CHAUMMA katika kipindi cha miaka mitano alikuwa mbunge, je alifanya nini? Kama hakufanya jiongezeni,”amesema Dk. Timo.
Amebainisha, kuwa mgombea huyo hawezi kuongoza Jimbo la Segerea hivyo anachofanya ni uchu wa madaraka.
“Alikuwa mbunge wa CHADEMA na ni bora angebaki ndani ya CHADEMA na kusubiri mwaka 2030 CHADEMA itakaposhiriki uchaguzi mkuu.
Hatuwezi kuingia katika uchaguzi kiujanja ujanja. Alikuwepo bungeni alipotoka kule alipaswa kustaafu,”amesema.
Ameewapongeza Halima Mdee na Anathopia Peter waliokuwa wabunge wa viti maalumu CHADEMA ambao waliamua kustaafu na kubaki CHADEMA hadi 2030.
“Hawa ndiyo wanachama shupavu. Ameeleza Dk. Timo.
Ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya mgombea ubunge huyo kueleza kuwa wanaohama chama hicho na kurejea CHADEMA ni vibaraka wanao lipwa fedha.
“Anadai sisi tuliohama CHAUMMA kwenda CHADEMA ni vibaraka. Tunatumwa kuichafua CHAUMMA na tuna lipwa.
Ni upotoshaji mkubwa,”ameeleza.
Anasema Agesta akumbuke alitoka CHADEMA kwenda CHAUMA yeye ni nani? Je, ni kibaraka na kuna watu walimlipa?.
“Anapozungumza kuwa tunalipwa basi hili ni suala la TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Huyu amekuwa mbunge kwa miaka mitano akiishi Segerea, lini alisaidia watoto wenye mahitaji maalumu? Lini alichangia hata kiti mwendokatika vituo vyetu vya afya?,”ameeleza.
Dk. Timo ameeleza inashangaza kuona Agnesta yuko Segerea na anachapisha fulana na kuhoji fedha anazitoa wapi.
“Mbona katika kipindi chote akiwa mbunge hakuweza hata kujitolea kujenga hata daraja la miti Segerea? Kinyerezi kwa Majoka kuna shida ya vivuko angejenga hata daraja la miti. Hakuna,”amebainisha.
Dk. Timo, ameeleza, ikiwa mgombea huyo ataendelea kumshambulia basi ataanika njama zote anazotumia kujijenga kisiasa.
“Tunawanachama wengi kutoka CHAUMMA wameamua kujiunga CHADEMA. Ninaipongeza CHADEMA wamenipokea kwa mikono miwili ila kuna shauri liko mahakamani la viongozi wa CHADEMA kutokutumia mali za chama ndiyo maana tukio hili hatukulifanyia kwenye ofisi ya CHADEMA, ”amesema.
Akizungumza kwa niaba ya waliokuwa wachama wa CHAUMMA waliokihama chama hicho jana, Aisha Abdalah, amesema, Agnesta anatumia sera ya kutoa mikopo ambayo kamwe hawezi kuitekeleza na wananchi wa Segerea wasidanganywe na sera hiyo.
Kupitia video ya Agnest aliyofanya kikao kwenye ofisi ya Kanda ya Segerea amesema Dk. Timo na wengine wanaohama chama hicho ni kwa masirahi yao binafsi.
Agnesta ameendelea kusema yeye kama binaadamu pamoja na kufanya mengi akiwa bungeni miongoni mwa watu aliowasaidia sana ni Dk. Timo.
Akisisistiza kauli hiyo amesema anakumbukumbu ya miamala ya fedha alizowahi kumsaidia Dk. kwa yeyote asiyeamini na kutaka kujionea miamala ya fedha alizokuwa akimsaidia kwenda kujionea kwenye simu yake.
“Huyo Dk Timo miongoni mwa watu niliowasaidia sana kama niloivyowahi kuwasaidia wengine na ushahidi wa miamala kwenye simu yangu nnao hivyo kama anahama kwa masirahi yake mimi siwezi kumzuia”. Alisikika akisema Agnesta kwenye video hiyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!