

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, leo amefanya mahojiano maalum na Global Radio kupitia Global TV, ambapo amejibu maswali na hoja nzito zinazohusu siasa za sasa nchini.
Katika mahojiano hayo, Golugwa aligusia kwa kina msimamo wa chama chake kuhusu kauli ya “No Reforms, No Election”, akibainisha kuwa CHADEMA haijairuka hoja hiyo kama inavyodaiwa, bali kinasimamia kwa dhati madai ya marekebisho ya mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha haki na usawa vinapatikana kabla ya kura kupigwa.
Aidha, Golugwa hakusita kugusia sakata linalomkabili Luhaga Mpina, ambalo limekuwa gumzo mahakamani leo. Alisema tukio hilo ni kielelezo cha changamoto kubwa zinazokumba mfumo wa kisiasa na kisheria nchini, akisisitiza kuwa haki lazima itendeke kwa kila mgombea bila upendeleo.
Kwa ujumla, mahojiano hayo yalionekana kuwa jukwaa la CHADEMA kuweka wazi msimamo wake, huku Golugwa akisisitiza kuwa chama hicho kipo tayari kupigania demokrasia ya kweli na hatimaye kushiriki uchaguzi wenye uwazi na haki kwa Watanzania wote.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!