
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni zake akiwa mkoani Songwe ambapo alikutana na maelfu ya wananchi wa Tunduma.
Akiwa jukwaani, Dkt. Samia aliwaomba Watanzania kushiriki uchaguzi kwa wingi na kuhakikisha wanakipigia kura ya ndiyo Chama Cha Mapinduzi kuanzia nafasi ya Urais, Wabunge hadi Madiwani. Kwa ishara ya kupiga simu, aliwasisitiza wananchi kupeleka salamu ya mshikamano na mshangao wa kishindo kwenye sanduku la kura Oktoba 29.
Kwa upande wao, wananchi wa Tunduma walimjibu kwa hamasa kubwa wakimthibitishia kuwa wapo tayari kumvusha kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao, wakisisitiza mshikamano wao na CCM na kuahidi kura za ndiyo kwa wagombea wote wa chama hicho.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!