Mamlaka za Taliban nchini Afghanistan zimeripoti kuwa idadi ya watu waliofariki katika tetemeko hilo la jumapili imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 1400, huku takriban watu elfu tatu wakijeruhiwa. Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa watu walikuwa wamelala wakati tetemeko hilo lilipotokea na hawakuweza kufika eneo salama katika jimbo la Kunar. Juhudi za uokoaji zimetatizwa na maporomoko ya ardhi yaliyofunga barabara katika maeneo ya milimani.
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!