AIR Manula amerejea ndani ya kikosi cha Azam FC akitokea kwa waajiri wake Simba SC akiwa mchezaji huru. Mkataba wa Air Manula na Simba SC ilikuwa mpaka 2025 tayari umegota mwisho.
Kwa msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya Azam FC, matajiri wa Dar mpaka 2028 akitimiza majukumu yake kwenye eneo la mlinda mlango.
Msimu wa 2024/25 akiwa ndani ya Simba SC hakupata nafasi kucheza mchezo hata mmoja wa ligi namba nne kwa ubora akigotea kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan alitumia dakika 45 pekee.
Ikumbukwe kwamba Air Manula alikuwa hapo 2012-17 alikuwa ndani ya kikosi cha Azam FC na lisajiliwa na Simba SC 2017-2015 amesepa akiwa mchezaji huru.
Rekodi yake yafikiwa na Camara
Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC aliifikia rekodi ya Aishi Manula katika kukusanya hati safi ndani ya uwanja kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Camara, Juni 22 2025 alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Kagera Sugar na aliokoa hatari mbili zilizokuwa zinakwenda langoni mwake ya kwanza ilikuwa dakika ya 24 ni Momo wa Kagera Sugar jaribio lake akiwa ndani ya 18 liliokolewa.
Dakika ya 42 Mahundi alifanya jaribio ambalo liligotea kwenye mikono ya Camara ambaye alipiga shuti lililolenga lango na mwisho ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukasoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar bao la Steven Mukwala dakika ya 17.
Ni hati safi 19 alifikisha Camara akiwa anaongoza katike eneo hilo huku anayemfuatia akiwa ni Djigui Diarra wa Yanga mwenye hati safi 17 msimu wa 2014/25.
Camara alifikia rekodi ya Aishi Manula ambayo aliiandika msimu wa 2017/18 alipokuwa kipa namba moja wa Simba SC ambaye kwa sasa atakuwa ndani ya Azam FC.
The post KUHUSU MANULA KURUDI ZAKE AZAM FC…HII HAPA STORI NYUMA YA PAZIA ISIYOSEMWA…. appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!