

Ni miaka tisa imepita sasa tangu kutokea kwa tukio lisilo la kawaida, lililozigusa hisia za wengi, tukio la kijana Said Mrisho, kuchomwa visu na kutobolewa macho na kijana mwingine, Salum Njwete almaarufu Scorpion, lililotokea Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam.
Scorpion yupo mtaani baada ya kumaliza kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani alichohukumiwa baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo lakini kwa upande wa Said aliyetobolewa macho, mambo hayajawahi kuwa sawa tena!
Kwenye mahojiano Said amefunguka kuwa ingawa alikuwa anafahamu kuwa ipo siku atakufa kama binadamu wengine, hakuwahi kufikiria kuwa kuna siku maisha yake yangebadilika ghafla na kuwa mlemavu.
Akaendelea kufunguka kuhusu maisha yake na kueleza kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, ni miongoni mwa watu waliowahi kumsaidia, hasa katika kipindi ambacho alikuwa na changamoto zinazohusu masuala ya kodi.
Tukio la kutobolewa macho, limebadilisha kila kitu kwenye maisha yake na sasa amekuwa ni mtu wa kuomboleza kila siku, mithili ya mtu mwenye msiba mzito.
Hapa anasimulia kuhusu ahadi zilizotolewa kipindi alipopata matatizo na utekelezaji wake.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!