Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump Apendekezwa Kwa Tuzo ya Nobel na Netanyahu

  • 36
Scroll Down To Discover

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemkabidhi Rais wa Marekani Donald Trump barua rasmi ya pendekezo lake la uteuzi kwa Tuzo ya Amani ya Nobel, akimsifu kwa juhudi zake katika kutafuta suluhu za Netanyahu migogoro ya Mashariki ya Kati.

Tukio hilo lilijiri jana Jumatatu, wakati wa mkutano wao Ikulu ya White House, Marekani, ambapo viongozi hao walijadili masuala ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas pamoja na athari za mashambulizi ya Marekani dhidi ya miundombinu ya nyuklia ya Iran.

Rais wa Marekani Donald Trump

Netanyahu alisema hatua hiyo ya uteuzi ni kwa kutambua mchango wa Trump katika kuendeleza mazungumzo ya amani, hasa kupitia ushirikiano na nchi nyingine kutafuta njia bora ya kuwawezesha Wapalestina kwa mustakabali bora. “Unastahili,” alisema Netanyahu alipomkabidhi Trump barua hiyo. Trump, kwa upande wake, alisema, “Inanigusa sana hasa kutoka kwako.”

Mkutano huo unafanyika katika wakati nyeti ambapo Marekani inatarajiwa kushinikiza Israel kukubali kusitisha mashambulizi Gaza, baada ya vifo vya takribani watu 60,000, wengi wao wakiwa Wapalestina. Maafisa wa Israel na Hamas walikutana Doha, Qatar, kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja, ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya wiki sita. Hata hivyo, tofauti bado zipo kuhusu dhamana za usalama na hatma ya Hamas Gaza.

Rais wa Marekani Donald Trump

Katika mazungumzo hayo, Netanyahu alisisitiza kuwa Wapalestina “wana haki ya kubaki au kuondoka Gaza kwa hiari yao” akikanusha madai ya Israel kupanga kuwahamisha kwa lazima wakazi wa Rafah. Alisisitiza kuwa Gaza haipaswi kuwa kama gereza, bali sehemu huru inayowapa watu chaguo la maisha bora.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Vodacom Yatumia Teknolojia ya Smart Screen Kutoa Elimu Sabasaba
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 09, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook