

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehutubia maelfu ya wananchi wa Msumbiji katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa taifa hilo. Sherehe hizo zimefanyika katika Uwanja wa Machava, jijini Maputo, kwa mwaliko maalum wa Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Daniel Francisco Chapo.
Katika hotuba yake, Rais Samia aliipongeza Msumbiji kwa hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa tangu kupata uhuru mwaka 1975, na kusisitiza uhusiano wa kihistoria, kindugu na kidiplomasia kati ya Tanzania na Msumbiji. Pia alisisitiza dhamira ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Msumbiji katika masuala ya maendeleo, amani, usalama na ustawi wa watu wa mataifa yote mawili.
Sherehe hizi zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Msumbiji, wakazi wa Maputo, pamoja na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali, ikiwa ni ishara ya mshikamano wa kimataifa kwa taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
Maputo, Msumbiji – Tarehe 25 Juni 2025
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!