Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM Yapiga Marufuku Shamrashamra uchukuaji na urejeshaji wa fomu za ubunge na udiwani

  • 15
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa mwongozo mpya wa kudhibiti shamrashamra na pilikapilika zisizo na ulazima wakati wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge na udiwani.

Kupitia taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Issa Haji Ussi, CCM imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda misingi ya umoja, mshikamano, na usawa miongoni mwa wanachama wake.

“Ni marufuku kwa mwanachama yeyote kualika kundi la wapambe, kuandaa msafara wa magari, pikipiki, baiskeli, ngoma, matarumbeta au aina yoyote ya shamrashamra katika kuchukua au kurejesha fomu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Ussi ameonya kuwa vitendo hivyo huibua viashiria vya makundi na mpasuko ndani ya chama, jambo ambalo halikubaliki kwa misingi ya maadili ya CCM.

Ameongeza kuwa chama kimeweka utaratibu wa usimamizi wa karibu wa mchakato mzima kuhakikisha kila mwanachama anafuata taratibu zilizowekwa, huku akibainisha kuwa mwanachama yeyote atakayekiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua za kinidhamu, ikiwemo kuondolewa sifa za kuteuliwa kuwa mgombea.

“Hatua hizi hazitachukuliwa kwa upendeleo wala uonevu, bali kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili ya CCM,” amesisitiza.



Prev Post FT: YANGA 2-0 SIMBA…..BUNDI ATUA MSIMBAZI…MASTAA JAGWANI KUJAZWA MINOTI….
Next Post Majaliwa: Rais Dkt. Samia Amekuwa Kiongozi Wa Kufanikisha Maendeleo Nchini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook