Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

PILATO MECHI YA DABI ‘ANAGUNDU’ NA SIMBA….CAF WALIMTOA GHAFLA MECHI NA STELLENBOSCH..

  • 30
Scroll Down To Discover

✍🏿.. ANAANDIKA NAZARETH UPETE

Niwapongeze mno @ligikuu kwa kuamua kuja na waamuzi kutoka nje ya Nchi hasa kwenye mchezo huu wenye maamuzi magumu na unaohitaji sana utayari wa waamuzi bora✅

Tumtazame mwamuzi wa kati:

Huyu ndiye alitakiwa kuchezesha mechi ya Stellenbosch vs Simba kule Afrika Kusini baadae akapata majeraha na kuondolewa ndio akaingia yule jamaa mwenye ‘Way’ kichwani. Kama mnakumbuka refa alibadilishwa ghafla basi ndiye huyu.

Amin Mohamed Oumar ni mzaliwa wa Septemba 25, 1985 pale Mohandsen, Cairo nchini Misri.

Alianza uamuzi rasmi wa Ligi Kuu Misri 2013 na alikuja kupata Benicia FIFA 2017 na amekuwa miongoni mwa waamuzi bora barani Afrika na Misri akifahamika kwa msimamo bayana na uaminifu kwenye kazi yake!

Wengi watamkumbuka kwa kadi nyekundu ya Grant Kekana mwaka Jana kwenye mchezo wa mshindi wa tatu wa AFCON baina ya Nigeria vs South Africa✅

Amechezesha mashindano mengi lakini kubwa ni Kombe la Dunia la chini ya miaka 17 (2019) kule Brazil. Pia alichezesha mchezo wa ufunguzi wa AFCON baina ya Ivory Coast dhidi ya Guinea Bissau.

Hii itakuwa mechi nyingine kwake kuchezesha Simba kwani alikuwa mwamuzi wakati Simba wakipoteza bao 1-0 dhidi ya Horoya Novemba 2, 2023 kwenye makundi ya CAF CL ✅

Ameshaichezesha pia timu ya Taifa ya Tanzania kwenye AFCON vs Congo DR iliyoisha kwa 0-0. Pia ameshachezesha michezo 17 ya CAF kwa upande wa Vilabu.

Kwenye michuano ya CAF ya timu za Taifa amechezesha mechi 6 akatoa kadi za njano 13 na kadi nyekundu 3 huku akitoa mikwaju 3 ya penati ✅😂

Nyumbani Misri!? Ameshachezesha mechi kubwa kuliko zote ya Al Ahly vs Zamalek kwenye Egypt Super Cup hatua ya Fainali.

Ni mwamuzi mpole ila mwenye ROHO NGUMU sana✅ Waambieni wachezaji wenye sukari hapa watadunda…! Hiki Chuma kutembeza umeme SIO SHIDA ZAKE!

The post PILATO MECHI YA DABI ‘ANAGUNDU’ NA SIMBA….CAF WALIMTOA GHAFLA MECHI NA STELLENBOSCH.. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KUELEKA DABI YA 25…, HUYU MUKWALA HUYU….’SHOW’ YAKE YANGA WAJIPANGE LA SIVYO 🫣🫣…
Next Post BASHIRI GG&3+ PSG VS SEATTLE SOUNDERS USHINDE MARA 2…..HII HAKUNA KUPOTEZA….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook