Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Hussein Mwinyi Achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM

  • 9
Scroll Down To Discover

Zanzibar, 30 Agosti 2025 – Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo amechukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Dkt. Mwinyi aliwasili katika ofisi za ZEC akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo:

Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Pius Chatanda (MCC)

Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Khamis Shomari (MNEC)

Katibu Mkuu wa UWT, Suzan Peter Kunambi (MNEC)

Pamoja na wananchi na wafuasi wa CCM waliojitokeza kumshuhudia.

Hatua ya Dkt. Mwinyi kuchukua fomu inamfanya kuwa miongoni mwa wagombea rasmi wa CCM kuelekea uchaguzi wa Urais wa Zanzibar, huku chama hicho kikiendelea na mchakato wa kidemokrasia kuhakikisha ushindani na upatikanaji wa mgombea wa kupeperusha bendera yake.

 



Prev Post Wananchi wa Gairo Wampokea Kwa Shangwe Dkt. Samia (Picha +Video)
Next Post Wazazi Waishtaki ChatGPT Wakidai Kusababisha Kifo cha Mtoto Wao
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook