Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wananchi wa Gairo Wampokea Kwa Shangwe Dkt. Samia (Picha +Video)

  • 6
Scroll Down To Discover

Gairo, Morogoro – 30 Agosti 2025 – Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amepokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi wa Gairo, mkoani Morogoro, akiwa njiani kuelekea Kibaigwa, Dodoma kuendelea na mikutano ya kampeni.

Wananchi wa Gairo walijitokeza kwa wingi barabarani na kwenye viwanja, wakimshangilia kwa nyimbo, mabango na salamu za upendo. Wameahidi kumpa kura nyingi za “Ndiyo” ifikapo Oktoba 29, 2025, wakisisitiza imani yao kwa uongozi wake unaoendelea kuwaletea maendeleo.

Dkt. Samia aliwashukuru WanaGairo kwa mapokezi hayo ya heshima, akiahidi kuendelea kusikiliza na kushughulikia kero zao kupitia sera na ilani ya CCM inayolenga kuboresha maisha ya kila Mtanzania.



Prev Post Majaliwa Ataka Mikakati Zaidi Matumizi Ya Nishati Safi Kwenye Magereza
Next Post Dkt. Hussein Mwinyi Achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook