Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

AZAM FC ‘WAKABA KOO’ ISHU YA FEI TOTO KUTUA SIMBA & YANGA….DAU JIPYA KUFURU…

  • 5
Scroll Down To Discover

NGOMA ni nzito kwa kiungo mshambuliaji Feisal Salum kusepa ndani ya Chamazi Complex kupata changamoto sehemu nyingine mpya kutokana na mabosi wa timu hiyo kuongeza dau upande wa mshahara.

Fei amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Simba SC na Yanga SC ambazo zinapigana vikumbo kusaka saini yake.

Ipo wazi kwamba Fei ni namba moja kwa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika akiwa ametengeneza jumla ya pasi 13 ndani ya kikosi cha Azam FC msimu wa 2024/25.

Azam FC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tatu kwa sasa ipo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa raundi ya 29 utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Juni 18 2025.

Mchezo huo utakuwa dhidi ya Tabora United kwenye msako wa pointi tatu muhimu katika kukamilisha mzunguko wa pili.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo ambaye mkataba wake umesalia mwaka mmoja mabosi wa Azam FC wapo kwenye mazungumzo naye ili aongeze mkataba mwingine hivyo ngoma itakuwa nzito kwa timu nyingine kupata saini yake.

The post AZAM FC ‘WAKABA KOO’ ISHU YA FEI TOTO KUTUA SIMBA & YANGA….DAU JIPYA KUFURU… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post AZAM FC ‘WAKABA KOO’ ISHU YA FEI TOTO KUTUA SIMBA & YANGA….DAU JIPYA KUFURU…
Next Post AZAM FC ‘WAKABA KOO’ ISHU YA FEI TOTO KUTUA SIMBA & YANGA….DAU JIPYA KUFURU…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook