
Kijana mwenye maono kama anavyoitwa na wengi, Nabii Simeon Malisa ambaye alichukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Kawe kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi katika Uchaguzi Mkuu ujao unatarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu jana ameirudisha rasmi tayari kwa kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza na mwanahabari wetu Malisa amesema tarehe rasmi ya kampeni ilikuwa bado lakini baada ya hapo anatarajia kuanza rasmi kunadi kampeni kampeni zake.
Malisa amewataka Wanakawe kuacha tabia ya kuwachagua viongozi kwa kuangalia ushabiki, ukubwa wa majina yao, chama vyama vyao na ushawishi mwingine usio wa kimaendeleo bali wajiandae kusikiliza kampeni zake zinazotekelezeka.
Alisema kijana huyo mwenye karama ya kinabii ambayo anataka kuitumia kwa ukombozi wa jimbo hilo.
“Kikubwa leo nimerejesha fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kawe, kupitia chama changu cha NCCR Mageuzi” Alisema jana Nabii Malisa.
#kawempyafursakwawote
#sautiyavijana
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!