Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Watu Waliofariki Kwa Mafuriko Nigeria Wafikia 115

  • 34
Scroll Down To Discover

Watu zaidi ya 115 wamepoteza maisha na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha katika jimbo la Niger, katikati mwa Nigeria, kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo siku ya Ijumaa.

Mafuriko yalimeza mji wa Mokwa baada ya mvua kuanza kunyesha usiku wa Jumatano na kuendelea hadi asubuhi ya Alhamisi. Ibrahim Audu Hussein, msemaji wa shirika la usimamizi wa dharura la jimbo hilo, alisema juhudi za uokoaji bado zinaendelea..

“Tayari tumepata miili 115 na tunatarajia kupata miili zaidi kwa sababu mafuriko yalitokea kutoka mbali na kuwasomba watu hadi Mto Niger. Hadi sasa, miili bado inaendelea kupatikana,” Husseini aliambia shirika la habari la AFP. “Hivyo basi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka.”

Zaidi ya nyumba 3,000 ziliripotiwa kufunikwa na mafuriko, aliongeza.

Mji wa Mokwa, ulio takribani maili 230 (kilomita 370) magharibi mwa mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ni kitovu cha biashara katika jimbo la Niger, ambapo wafanyabiashara na magari makubwa ya mizigo husafirisha bidhaa kwenda maeneo mengine.

Stori: Elvan Stambuli, GPL

RAIS SAMIA ANATUNUKIWA TUZO MAALUM NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA – DODOMA…



Prev Post Rais Samia Apokea Tuzo Maalum Kutoka Bunge La Tanzania (Picha +Video)
Next Post Ukaguzi Wa Mabasi Ya Abiria Wafanyika Kudhibiti Ajali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook