Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

John Heche Aongoza Ziara ya Kumbukizi kwa Hayati Ndesamburo

  • 34
Scroll Down To Discover

Kilimanjaro, Mei 30, 2025 – Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, leo ameongoza ujumbe wa viongozi wa chama hicho katika ziara maalum ya kuzuru kaburi la hayati Mzee Philemon Ndesamburo, mmoja wa waasisi wa CHADEMA na mwanasiasa mkongwe aliyefariki dunia tarehe 31 Mei 2017.

Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya shughuli za chama hicho katika mikutano ya hadhara ya Kanda ya Kaskazini, ambayo imekuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Manyara.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya heshima, Heche alisema:

“Mzee Ndesamburo alikuwa nguzo ya kweli ya CHADEMA. Alisimamia misingi ya demokrasia kwa ujasiri, hekima na moyo wa kujitolea. Tumekuja hapa leo si tu kumkumbuka, bali kujikumbusha sisi sote wajibu wetu kwa Taifa.”



Prev Post MUME ALIVYOMUOKOA MKEWE KUFANYIWA UPASUAJI AKIJIFUNGUA
Next Post Jica Yaahidi Kuendelea Kuishika Mkono Serikali Ya Tanzania – Majaliwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook