
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Viongozi na wanachama wake kisiwani pemba kujiandaa kisaikolojia na kujipanga kimkakati tayari kushiriki uchguzi mkuu wa oktoba mwaka huu
Pia chama hicho kimesema Uchaguzi si jambo dogo bali ni mapambano ya sera na hoja si kama kucheza lelelmama au singeli.
Maelezo hayo yametolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis , alipozumgumza na makundi ya viajna Wahamasishaji na Wasanii katika Ukumbi wa Makonyo huko Wawi Kisiwani hapa.
Mbeto alisema kila kiongozi na Mwanachama kwa nafasi zao, wanatakiwa kuhahakikisha wanafanya kila linalowezekana ili kupata ushindi wa kidemokrasia kwa kuwahamasisha wanachama na wananchi.
Alisema matokeo ya ushindi wa uchaguzi ni baada ya chama kutangaza sera zake ,wananchi kupiga kura ,kuhesabiwa na matokeo kutangazwa.
Alisema ni matarajio ya kila chama cha siasa kipate idadi kubwa ya kura ,kwakuwa wala Uchaguzi si simulizi za hadithi au maneno matupu.
‘Chama chenu kinawataka viongozi wote mjipange na kujiandaa kimkakati kuelekea Oktoba Mwaka huu. Uchaguzi umeshapiga hodi hivyo lazima tukumbushane mapema na kuanza kujipanga “Alisema Mbeto.
Aidha ,alisem pamoja na kila unapomalizika uchaguzi mkuu mmoja , CCM hujiandaa kwa uchaguzi mwingine, aliwataka wanachama kutobweteka na kufanya mambo kwa mazoea.
“Uchaguzi hubadilika kulingana na mazingira husika.Hata Malaria ukipima utakuta idadi ya juu au ya chini ya wadudu wake.Uzoefu katika kila uchaguzi una uzoefu na mazingira yake “Alisema Mbeto
Hivyo basi, Katibu huyo Mwenezi alisema hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi peke yake bila kuwashirikisha wenzake huku akiwataka viongozi wa CCM kushirikiana na wanachama wao.
“Wasanii jiandaeni kutunga mashairi ya nyimbo nzuri za hamasa na kampeni .Wahamasishaji lazima mpite kila nyumba, kiambo kwa kiambo,shehia hadi shehia kuomba kura kwakuwa huo ni wajibu wa kidemokrasia “Alieleza
Alisema nyimbo zote zitakazotungwa zitahakikiwa mapema na kupasishwa kabla ya kuimbwa , hivyo aliwataka watunzi wa nyimbo hizo kuanza kutunga mashairi yatakayovutia na kuelimisha wananchi kuhusu uchaguzi mkuu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!