
Dodoma, Agosti 26, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba mara baada ya kuapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
Rais Samia alisisitiza umuhimu wa viongozi hao kushirikiana na wananchi na kuhakikisha utekelezaji wa sera na miradi ya maendeleo unafanyika kwa ufanisi katika ngazi zao mbalimbali. Hotuba hiyo pia ilisisitiza mshikamano wa kitaifa, uwajibikaji na kuzingatia maadili mema katika utumishi wa umma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!