
Dodoma, Agosti 26, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuapisha CPA Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Hafla ya kumsimika Makalla ilifanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na mamlaka za mkoa walishiriki.
Makalla ataanza rasmi majukumu yake ya kusimamia maendeleo na uendeshaji wa shughuli za serikali mkoani Arusha, akilenga kuhakikisha ushirikiano mzuri kati ya serikali, wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!