Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MASHINE MBILI MPYA SIMBA HIZI HAPA….’MAJAMAA’ YANAPIGA KAZI HATARI…..

  • 2
Scroll Down To Discover

SIMBA inaendelea kujifua kambini jijini Cairo, Misri chini ya kocha Fadlu Davids, lakini kuna mashine mbili mpya zinasubiriwa huko ili kuungana na wenzao walitangulia mapema.

Awali Simba ilipiga kambi ya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya katika mji wa Ismailia, kisha ikahamia Cairo ilipo kwa sasa ikiwa imeshacheza mechi kadhaa za kirafiki za kujipima nguvu, lakini kuna mastaa wawili wanadaiwa wameshasaini mkataba kitambo wakiwa Dar es Salaam.

Nyota hao ni kipa Yakoub Suleiman na beki Wilson Nangu waliokuwa katika majukumu ya Taifa Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN) 2024 wakitokea klabu ya JKT Tanzania, inadaiwa kwa sasa wanasubiri simu za mabosi wa timu hiyo, ili kujiunga na Simba.

Ipo hivi. JKT Tanzania ilitoa sharti kwa Simba ili iwaruhusu Nangu na Yakoub kujiunga nao, ilitakiwa itoe pesa na wachezaji watatu kwa mkopo ambao ni David Kameta ‘Duchu’, Awesu Awesu na Valentino Mashaka ambao wapo kambini nchini Misri.

Chanzo cha ndani kimesema kuwa kuhusu Nangu na Yakoub bado hawajaambiwa chochote na uongozi wa JKT Tanzania kama watatakiwa kuondoka kwenda Misri kujiunga na Simba, ukimya huo utawalazimu wachezaji hao kwenda katika kambi ya Arusha.

“Simba ilifanya mazungumzo na JKU ambayo ni mwaajiri wa Yakoub kijeshi, lakini iliambiwa iingize pesa kwa mchezaji, JKU na JKT Tanzania ambayo ilikuwa na kipa huyo aliyemaliza msimu uliyopita na clean sheets 10 sasa jukumu la kumruhusu mchezaji lipo kwa JKT,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kuhusu Nangu mwenye mkataba wa kumalizika mwaka 2028 moja ya sharti ni Simba kuwatoa wachezaji wao kwa mkopo, hivyo bado JKT Tanzania ndiyo inatakiwa iwaruhusu kuondoka.”

Klabu ya Simba imetajwa kumalizana na wachezaji hao na walikuwa wakiwasubiri wamalize majukumu yao na Taifa Stars iliyotolewa robo fainali ya CHAN 2024 ili wapandishwe ndege kuwahi kambi iliyopo jijini Cairo, Misri chini ya kocha Fadlu Davids.

The post MASHINE MBILI MPYA SIMBA HIZI HAPA….’MAJAMAA’ YANAPIGA KAZI HATARI….. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BAADA YA KUMALIZANA NA CHAN….TSHABALALA APEWA SIKU 5 YANGA….FOLZ HACHEKI NA MTU …..
Next Post Wanahabari 5 wauawa katika shambulizi la Israel huko Gaza, katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook