Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jeshi la Polisi Lachunguza Tukio la Risasi Inayomuhusisha Dogo Janja Arusha

  • 3
Scroll Down To Discover

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mgombea udiwani kata ya Ngarenaro kupitia CCM, Abdulaziz Abubakari Chande maarufu kama “Dogo Janja”, alitumia silaha yake akijihami katika tukio lililosababisha kijana mmoja kujeruhiwa kwa risasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo, tukio hilo lilitokea Agosti 23 majira ya saa 5:30 usiku katika maeneo ya Sombetini, jijini Arusha, ambapo Bakari Halifa Daudi (18) alijeruhiwa kwa risasi mguuni.

 

 

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wakati Abdulaziz akishuka kwenye gari, alidai kuwa alitaka kuvamiwa na Bakari akiwa na mwenzake wakiwa na silaha za jadi. Hali hiyo ilisababisha mtuhumiwa kutumia silaha yake na kumpiga risasi Bakari,” imesema taarifa hiyo.

Kamanda Masejo amethibitisha kuwa polisi wamewakamata watu wawili kuhusiana na tukio hilo na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini undani wa tukio na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa.

Bakari kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu kutokana na jeraha alilopata.



Prev Post Kirumbe Shaaban Ng’enda Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi CCM
Next Post FADLU AIFUMUA SIMBA UPYAAA…..MASTAA SABA WAPYA SIO POA….KIBU , AHOUA MHHHH…..
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook