Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Infocus Studio waiwakilisha Tanzania kwa Kishindo Katika Kongamano la CABSAT Dubai

  • 37
Scroll Down To Discover

Dubai, Falme za Kiarabu – Mei 16, 2025, Joshua Moshi, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Infocus Studio, ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kushiriki kama mzungumzaji katika jukwaa la kimataifa la teknolojia ya utangazaji lililoandaliwa na kampuni ya YoloLiv kwenye kongamano la CABSAT 2025 lililofanyika Dubai.

Katika tukio hilo lilowakutanisha wataalam na wabunifu wakuu wa teknolojia ya utangazaji duniani, Joshua alizungumza kuhusu mada yenye kaulimbiu “Upgrade is Essential”, akieleza safari ya Infocus Studio kutoka kutumia vifaa vya kawaida hadi kuwa moja ya kampuni zinazoaminika zaidi kwa kurusha matukio ya kitaifa na kimataifa kwa ubora wa hali ya juu.

Joshua aliweka wazi umuhimu wa kuwekeza katika ubunifu na teknolojia rafiki kwa mazingira ya Afrika, akieleza kwa undani namna Infocus Studio ilivyoweza kuboresha huduma zake kwa kutumia vifaa kama Zamunda, YoloBox, ambavyo vimeleta mapinduzi katika namna ya kurusha matukio mubashara kwa wepesi, kasi na ubora unaohitajika kwenye majukwaa ya kimataifa.

Shukrani kwa Serikali ya Tanzania

Kupitia mafanikio haya, Infocus Studio imetoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuamini vijana na kampuni za ndani kushiriki katika miradi ya kitaifa.

Infocus Studio imepata fursa ya kihistoria kurusha mubashara matukio ya ngazi ya juu kama:

  • Mikutano mbalimbali iliyomuhusisha Mheshimiwa Raisi
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi – Human Capital Summit
  • Mkutano wa AGRF Summit 2023
  • Generation Equality Meeting kwa ushirikiano na UN Women na IMF
  • Hafla mbalimbali za CRDB Bank, Vodacom pamoja na World Bank.

Ushiriki wa Joshua katika kongamano la CABSAT ni uthibitisho kwamba vijana wa Kitanzania wanaweza kushindana na kushirikiana na dunia kwenye sekta za teknolojia na ubunifu, na Infocus Studio ni mfano hai wa mafanikio hayo.

Kuhusu Infocus Studio

Infocus Studio ni kampuni ya uzalishaji wa maudhui ya kidigitali yenye makao yake Dar es Salaam. Ikiwa mstari wa mbele katika huduma za livestreaming, multi-camera production na matangazo ya moja kwa moja, kampuni hii imejipatia heshima kama “Live Stream Kings” kutokana na ubunifu na weledi wake unaokidhi viwango vya kimataifa.



Prev Post Mradi wa Maendeleo ni Matokeo ya Usimamizi Mzuri wa Rasilimali
Next Post Ado Shaibu: Yeyote ACT Wazalendo rukra kugombea na vigogo kwnye chama
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook