
MAGAZETI ya Leo Jumamosi 17 May 2025
MAGAZETI ya Leo Jumamosi 17 May 2025
Kuanzia msimu wa masomo wa mwaka 2025/26, waombaji wa mikopo katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) watalazimika kuwa na namba (NIN) au kitambulisho cha Taifa.
Kuwa na NIN au kadi ya NIDA limewekwa kuwa takwa la lazima kwa kila mwombaji wa mkopo kupitia HESLB, kwa lengo la kurahisisha utambuzi wa mwombaji na usimamizi wa mikopo inayotolewa kwa wanufaika.
Utekelezaji wa takwa hilo unaanza na wanafunzi wa kidato cha sita ambao wamemaliza mitihani yao ya Taifa, ambao miezi michache ijayo baada ya matokeo kutoka, wanatarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu na ya vya kati.
Kwa mujibu wa mamlaka, mwombaji ambaye hatakuwa na NIN hataweza kuomba mkopo, hivyo kushindwa kupata huduma nyingine zozote ikiwamo kufungua akaunti za Benki.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!