Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wizi wa kipochi cha Waziri wa Usalama Marekani Wazua Kizaazaa!

  • 35
Scroll Down To Discover

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani, Christie Noemi ameibiwa kipochi chake wakati alipokuwa kwenye chakula cha jioni katika mkahawa mmoja mjini Washington.

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo tovuti ya habari ya televisheni ya CNN vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ndani ya kipochi hicho mlikuwa na pasipoti yake, beji ya usalama ya idara yake na pesa taslimu dola 3,000 za Kimarekani.

Kupanda gharama za maisha na kupungua uwezo wa manunuzi ya bidhaa kwa wananchi wa Marekani kumeongeza vibaka na kupandisha juu kasi ya wizi na vitendo vya uporaji nchini Marekani kwa asilimia 24. Maduka mengi sasa yameamua kuweka bidhaa zao kwenye vifurushi vilivyofungwa ili kukwepa wizi na uporaji na kukabiliana na vibaka.

Vita vya ushuru vilivyoanzishwa na Trump kote duniani katika wiki za hivi karibuni vimeongeza wasi wasi kuhusu hali mbaya ya uchumi nchini Marekani, na baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa kutokana na kupanda mfumuko wa bei, viwango vya wizi na uhalifu nchini Marekani vitaongezeka sana.

Ahadi za Donald Trump za kupunguza wizi na uhalifu nchini Marekani si tu ni ahadi chapwa, lakini pia watu wake muhimu ndani ya baraza la mawaziri nao hawajasalimika na wizi na uhalifu.

Stori: Elvan Stambuli



Prev Post Mwili wa Hayati Cleopa Msuya Waagwa Kwa Heshima Mwanga, Kilimanjaro – Picha
Next Post Mwili Hayati Cleopa David Msuya ulivyowasili Mwanga, Kilimanjaro leo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook