MAGAZETI ya Leo Jumatatu 12 May 2025
Uongozi wa Kampuni ya Harmonize Ent. Ltd kupitia Lebo yake ya Konde Gang Music Worldwide imetangaza kumsimamisha rasmi Msanii wake, Ibrahim Abdallah Nampunga (Ibraah), kutoa na kushiriki katika shughuli zozote za muziki kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wake na lebo hadi pale suala lake litakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa mujibu wa mkataba wake na sheria za Tanzania sababu ikiwa ni Ibraah kutoa machapisho ambayo yanamvunjia heshima Harmonize ambaye ni Boss wa lebo hiyo.
Lebo hiyo imempiga pia marufuku Ibraah dhidi ya kuchapisha, kutamka, au kufanya mawasiliano yoyote kuhusu suala hili kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii (kama vile Instagram, WhatsApp, Facebook, n.k.)
“Hii ni pamoja na mawasiliano ya aina yoyote ambayo yanaweza kuharibu taswira ya lebo au kumdhalilisha Mkurugenzi Muwekezaji wa lebo ambaye ni Msanii (Harmonize)”
“Tunatoa onyo kali kwamba iwapo haya yatakiukwa, lebo haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi yake katika Mahakama za Tanzania” (swipe kusoma zaidi)
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!