

Dar es Salaam, 23 Agosti 2025: Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) katika kuelekea Mkutano wao Mkuu wa Mwaka wanaenda sambamba na kufanya matendo ya huruma kwa kutoa misaada kwa jamii.
Leo wanachama wa taasisi hiyo wamepeleka misaada ya vitu mbalimbali kwa wagonjwa wa kansa wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Jijini Dar.
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Agosti, 23,2025 jijini Dar-es-Salaam, Mwenyekiti wa chama Cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) Devotha George Mrope amesema kuwa wamekuja ili kuungana jamii kwa ajili ya kuunga mkono kazi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameboresha kwa huduma za afya katika vituo vya vingi vya afya hivyo wao wametambua na kuona mabadiliko makubwa sana kwenye afya kwa kipindi cha usingizi wake.
Devota aliendelea kusema;
“Tumekuja hapa kuwafariji, kuwatembelea, kuwasaidia wagonjwa ambao wapo hapa na pia jana tulianza kwenye kitengo cha wagonjwa wa moyo hospital ya Muhimbili ambapo pia tuliwapa faraja.
“Kazi anayoifanya Rais kwa kuwekeza kwenye Afya ya binadamu ni kazi ya muhimu ya msingi na sisi kama sehemu ya Serikali tunaunga mkono ndio maana tupo hapa kufariji wenzetu na sisi pia tunatambua sisi.
“Leo ni wazima lakini sisi ni wagonjwa wa kesho hivyo tunatamani siku tukiwa wagonjwa tupate watu wa kutufariji na kututia moyo lakini tendo hili pia ni la kiimani kwa dini zote zinasisitiza kwamba hii ndio ibada iliyokuwa njema na Ibada ni bora.
Hivyo yeyote yule mwanachama wa TRAMPA iwe mfano popote pale alipo kwamba na anatakiwa atoe ili wenzetu waweze kupata faraja kutoka kwetu.
Kuanzia tarehe 25 mpaka 28 mwaka huu kutakuwa na Mkutano Mkuu wa mwaka ambao utafanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Kassim na kauli Mbiu yetu ya mwaka huu ni “Matumizi ya Ofisi Mtandao ni Chachu kufikia malengo makuu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025-2050.’
Nae Msimamizi wa Kitengo cha Kumbukumbu na Nyaraka kutoka Ocean Road, Wamoja Musa Mbonde akizungumza kwenye tukio hilo amesema anaishukuru sana Taasisi ya TRAMPA kwa kwenda kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji.
Amesema kitendo hicho kinawapa faraja kwa sababu wagonjwa wengi wanapata tiba kwenye taasisi hiyo wanatokea mikoa mbalimbali hivyo hawana wafariji wa karibu hivyo wao wamekuwa ndiyo wafariji wao hivyo wanashukuru sana.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!