MAGAZETI ya Leo Jumanne 06 May 2025
Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa mechi ya marudiano ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma amethibitisha kuwa Fainali ya Simba na RS Berkane itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi bungeni Jumatatu Mei 5, 2025, Naibu Waziri huyo amesema kila kitu kimekaa sawa na tayari ameshazungumza na viongozi juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) akiwamo rais Patrice Motsepe.
“Nataka kuwahakikishia kuwa, Fainali hiyo itapigwa katika uwanja wa Mkapa na hakuna namna nyingine. Tumeajili Mkandarasi kwa dharura na jana usiku nimeongea na Motsepe na kukubaliana kuwa Fainali itapigwa hapo,”amesema Mwinjuma.
Simba itakutana na RS Berkane ya Morocco Katika mchezo wa Fainali, huku mechi ya kwanza ikichezwa Morocco May 17 na mechi ya Fainali ya Pili itachezwa May 25,2025 hapa hapa Tanzania.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!