Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Kupinga Uteuzi wa Rais Samia

  • 29
Scroll Down To Discover

Dkt. Godfrey Malisa

Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia Masjala Kuu ya Dodoma, Agosti 22, 2025 imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyokuwa ikipinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Dkt. Godfrey Malisa, mkazi wa Moshi, dhidi ya Wadhamini wa CCM na Katibu Mkuu wa chama hicho.

Jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Joachim Tiganga, na kuhusisha Majaji Everisto Longopa na Griffin Mwakapeje, lilibaini dosari kadhaa za kisheria ikiwemo ukiukwaji wa masharti ya Katiba, kutokufuata taratibu za uchaguzi ndani ya CCM, pamoja na upungufu katika nyaraka za kiapo.

Miongoni mwa kasoro zilizojitokeza ni tofauti za majina ya mlalamikaji katika nyaraka zilizowasilishwa, hali iliyotia shaka uhalali wa kiapo hicho.

Kutokana na mapungufu hayo, mahakama iliamua kesi hiyo haina msingi thabiti wa kisheria na hivyo ikaifuta rasmi.



Prev Post Rais Samia Amtembelea Dr. Mabodi Hospitalini Dodoma
Next Post Wawili Wauawa Kwa Kuchomwa Moto Songwe
Related Posts
© Image Copyrights Title

Wawili Wauawa Kwa Kuchomwa Moto Songwe

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook