

Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Walusanga Ndaki amefariki dunia.
Taarifa kutoka kwa familia yake, zinaeleza kuwa Walusanga alifikwa na mauti jana, April 28, 2025 kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Enzi za uhai wake, Walusanga amewahi kufanya kazi kwenye magazeti ya Urusi Leo na The Guardian kabla ya kujiunga na familia ya Global Publishers.
Msiba wa Walusanga upo Gongolamboto (Moshi Bar) na anatarajiwa kuzikwa kesho, April 30, 2025.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!