Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita, huko Ofisini kwake Migombani Wilaya ya Mjini wakati alipopokea Ugeni wa Wanamitindo saba (7) kutoka Taasisi ya Miss Grand Tanzania Organization ambao wanataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Urembo Duniani katika Nchi mbalimbali.
…………….
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita amewataka Wanamitindo kuiwakilisha vyema Nchi kwa kutangaza Utamaduni wa Tanzania na lugha ya Kiswahili kwa Ujumla.
Ameyasema hayo, alipopokea akizungumza na Wanamitindo saba (7) kutoka Taasisi ya Miss Grand Tanzania Organization wakati walipofika Ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kujitambulisha.
Amesema, Ugeni huo, uliowasili Zanzibar, unaiwakilisha Nchi kwenye mashindano makubwa ya Urembo Duniani hivyo amewataka kutosahau kuitangaza Nchi yao kiutamaduni na kiutalii ikiwemo mavazi ya kanga na Chakula cha asili.
Amewataka Wanamitindo hao, kuitumia fursa hiyo kwa kukuza mahusiano mazuri na mataifa mengine ili kuitangaza Nchi ya Tanzania kiutalii na kiutamaduni.
Hata hivyo Waziri Tabia, aliwataka Warembo hao, kuwaungamkono Vijana wa Zanzibari ambao wanajishighulisha na Masuala ya faction design ili wapate muamko katika kufuatilia fursa ya kuingia katika mashindano hayo.
Sambamba na hayo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi wamekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono wabunifu mbalimbali ikiwemo wanamitindo ili kuutangaza Utamaduni wa Tanzania kiutalii.
Nae Katibu wa Miss Grand Organization Tumaini Henry, lengo la ziara hiyo ni kuunga mkono maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kudumisha Urithi wa Utamaduni wa Taifa pamoja na kutengeneza Filamu ya makala (documentary), itakayoonesha urithi wa Zanzibar kupitia Sanaa, Michezo na Uamaduni kwa ajili ya matumizi ya kimataifa.
Amesema Jumla ya Warembo saba, wameibuka ushindi kati ya warembo 24 ambao wamepata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa ya Urembo wa Dunia.
Miss Grand Tanzania ni Organization isiyokua ya kiserikali yenye lengo la kuwezesha warembo Wenye ndoto za kushiriki mashindano ya Urembo kimataifa na kuiwakilisha nchi kwa kupitia platform hii wanapata fursa Mbali mbali za kiuchumi pamoja na kuonesha vipawa vyao.
Miss Grand organization ipo Chini ya Kampuni y MISNAZI ENTERTINMENT COMPANY na Mkurugenzi NAZIMIZYE ADAM MDOLO
Kampuni Hii Ndo yenye dhamana ya kusimamia mashindano haya hapa nchini
Warembo watakaoshiriki katika Mashindano mbalimbali ni Beatrice Alex – Miss Grand Tanzania (Thailand), Jesca Michael – Miss Cosmo Tanzania (Vietnam), Amina Jige – Miss Earth Tanzania (Philippines), Efranzia Makene – Miss Elite Tanzania (Egypt), Faidha Kassim – Miss Intercontinental Tanzania (Egypt), Adelina Mapicha – Miss Tourism Africa (Nigeria).
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!