Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Papa mpya wa Kanisa Katoliki kuanza safari zake kimataifa na Lebanon

  • 2
Scroll Down To Discover

Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza ya kimataifa nchini Lebanon baadaye mwaka huu, ikiwa ni safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuchaguliwa mwezi Mei.

Askofu Mkuu Paul Sayah, mmoja wa viongozi wakuu wa Kanisa Katoliki nchini Lebanon, amethibitisha kwamba Vatican bado “inatathmini” mpango huo huku tarehe rasmi ikisubiriwa.

Ziara hiyo inatarajiwa kuwa na umuhimu wa kipekee, kwani Papa Leo ambaye ndiye Papa wa kwanza kutoka Marekani ameweka msisitizo mkubwa juu ya amani Mashariki ya Kati na mshikamano wa kidini.

“Lebanon ni nchi yenye tamaduni nyingi, yenye dini nyingi na ni mahali pa mazungumzo. Ni moja ya mazingira adimu ambapo Waislamu na Wakristo wanaishi pamoja na kuheshimiana… hivyo inatuma ujumbe kwa ukanda huo,” alisema Askofu Sayah.

Katika historia ya Kanisa Katoliki, safari za kwanza za mapapa mara nyingi huashiria vipaumbele vya uongozi wao. Kwa mfano, safari ya kwanza ya Papa Francis nje ya Roma mwaka 2013, kwenda kisiwa cha Lampedusa nchini Italia, iliweka msisitizo wake katika masuala ya uhamiaji na jamii zilizotengwa.

Kwa kipindi cha miaka 12 akiwa kiongozi wa Kanisa, Papa Francis alitembelea nchi 68 katika ziara 47 za kimataifa, mara nyingi akichagua maeneo yenye changamoto za kijamii na kiuchumi.

Lebanon yenye zaidi ya Wakatoliki milioni mbili na jamii zenye mchanganyiko wa kidini, imekuwa na nafasi ya kipekee kwa Kanisa kwa miongo mingi. Ziara ya Papa Leo huko pia inaweza kumuweka karibu zaidi na mzozo unaoendelea Gaza pamoja na mvutano wa muda mrefu kati ya Israel na Palestina.

Papa Leo tayari ameonyesha dhamira ya kuimarisha mazungumzo ya kidini, akisisitiza umuhimu wa Wakristo, Wayahudi na Waislamu “kusema hapana kwa vita na ndio kwa amani.”



Prev Post Binti Aliyeishi Mitaani Awashangaza Wengi kwa Kuendesha Range Rover
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 22, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook